1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul:Jaribio jengine la nyuklia lahofiwa.

18 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDKX

Serikali ya Korea ya Kusini inaichunguza ripoti ambayo inayopendekeza kwamba mapema Korea ya Kaskazini inawezekana ikawa na jaribio la Nyuklia la chini ya ardhi.

Kituo cha televisheni cha nchini Marekani kijulikanacho kama ABC kimesema, wana usalama wa Marekani wamebaini kile kilichokuwa kikizungumzwa ni kama harakati za shaka katika mradi wa nyuklia kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya kikomunisti.

Serikali ya rais Bush imepunguza makali taarifa hiyo kwa kusema kwamba maelezo yaliyotolewa hayana ushawishi wa kutosha kuweza kuaminika.

Mwaka uliopita Pyongyang ilitangaza kuwa inanguvu za Nyuklia.