1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal yazindua uwanja mpya baada ya AFCON

23 Februari 2022

Maelfu ya Wasenegal walikusanyika Jumanne jioni kwa uzinduzi wa uwanja wa michezo wenye uwezo wa kuwa na mashabiki 50,000. Uwanja huo unalenga kuifanya Senegal kutumika kama mwenyeji wa hafla za kimataifa.

https://p.dw.com/p/47UDj
Senegal | Eröffnung Diamniadio Olympia Stadion
Picha: Seyllou/AFP/Getty Images

Maelfu ya Wasenegal walikusanyika Jumanne jioni kwa uzinduzi wa uwanja wa michezo wenye uwezo wa kuwa na mashabiki 50,000. Uwanja huo unalenga kuifanya Senegal kutumika kama mwenyeji wa hafla za kimataifa. Uwanja huo upo Diamniadio, mji unaojengwa karibu kilomita 30 kutoka mji mkuu Dakar, ambapo safari za treni ya moja kwa moja ilizinduliwa Desemba mwaka jana. Dimba hilo, ambalo litapewa jina la rais wa zamani Abdoulaye Wade, utakuwa uwanja pekee nchini Senegal wenye idhini ya kutumika kwa mashindano ya kimataifa ya kandanda. Rais wa Senegal Macky Sall alisema wakati wa uzinduzi huo kuwa kutoa jina kwa uwanja huo ni heshima kwa mwanasiasa aliyepigania haki za Waafrika. Senegal walishinda Kombe la Afrika - AFCON kwa mara ya kwanza mwezi uliopita nchini Cameroon.