1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Salah arejea Liverpool kwa matibabu

22 Januari 2024

Mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Misri, Mohammed Salah, ameondoka katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika na kurejea katika klabu yake ya Liverpool kwa ajili matibabu.

https://p.dw.com/p/4bWtS
AFCON | Senegal vs. Misri| Mohamed Salah
Mohamed Salah alazimika kurejea Uingereza kwa matibabu.Picha: Ayman Aref/NurPhoto/picture alliance

Kwa mujibu wa klabu hiyo ya Ligi ya Premier, mshambuliaji huyo mwenye ushawishi kikosini alilazimika kuondoka uwanjani katika kipindi cha kwanza cha mechi iliyomalizika kwa sare ya 2 - 2 na Ghana siku ya Alhamis (Januari 19) hali iliyozusha wasiwasi kwa klabu na nchi yake. 

Wakati huo huo, duru ya mwisho ya mechi za makundi inaanza kuchezwa leo jioni ambapo katika Kundi A, Guinea Bissau itavaana na Nigeria wakati Guinea ya Ikweta itachuana na Cote d'Ivoire.  

Guinea ya Ikweta na Nigeria zina pointi nne kila mmoja wakati Cote d'Ivoire ina tatu.

Baadaye usiku, Msumbiji itaikaribisha Ghana katika Kundi B. Kila mmoja ana pointi moja.

Cape Verde wana alama sita na tayari wameshafuzu hatua ya mtoano wakati Misri ni ya pili na pointi mbili.