1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sakata la Loliondo laibuka tena bungeni Dodoma

Deo Kaji Makomba
20 Juni 2022

Mabishano makali yameibuka bungeni kufuatia sakata linaloendelea wilayani loliondo kaskazini mwa Tanzania huku mbunge Christopher Olesendeka wa CCM akisema kinachoendelea Loliondo ni batili.

https://p.dw.com/p/4Cx9m
Maasai aus Loliondo in Tansania
Picha: Judith Fehrenbacher

Hali hiyo imemuibua spika wa bunge la Tanzania Tulia Ackson kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kueleza ubatili huo unatokea wapi. 

Kauli hiyo imetolewa na Christopher Ole Sendeka mbunge wa Simanjiro kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, wakati akichangia hali ya uchumi wa taifa pamoja na bajeti kuu ya serikali iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita.

Tanzania - Serengeti und Loliondo
Masai akichunga ng'ombe wake LoliondoPicha: DW/A. Mittal

Akichangia, Ole Sendeka amesema kuwa mambo yanayoendelea katika maeneo ya Loliondo na sare ikiwemo kuchukua ardhi ya vijiji vya kata saba na kuunda pori tengefu la Loliondo ni ubatili.

Aidha Ole Sendeka ameongeza kusema kuwa licha ya yale yanayoendelea Ngorongoro na Loliondo, waziri mwenye dhamana ya maliasili na utalii nchini Tanzania, haoni jeraha hilo kwa jamii ya wafugaji wa kimaasai na ametangaza kuifanya Simanjiro kwa ujumla wake kuwa pori la akiba huku wananchi wasijue wanakwenda wapi.

Unajua ulikotokea mvutano wa Loliondo?

Kauli hiyo ya Ole Sendeka ilimfanya naibu waziri wa maliasili na utalii Mery Masanja kutoa ufafanuzi kuhusiana na kauli hiyo huku akisema kuwa hotuba ya waziri wa maliasili iligusia maeneo ambayo hayatahusisha vijiji vya wananchi na kuongeza kuwa. Soma pia Hatua ya Tanzania kuwaondoa Wamasai yazidi kuibua hisia

Kwa upande wake spika wa bunge la Tanzania Tulia Ackson alimtaka mbunge Ole sendeka kama ana uhakika na anachokisema awasilishe ushahidi wake.

Katika siku za hivi karibuni, serikali ya Tanzania imekuwa ikiendesha zoezi la uratibu na kuwahamisha kwa hiari wananchi wa maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kuweka alama katika eneo la Loliondo ili kuendeleza ikolojia na uhifadhi wa wanyama pori nchini Tanzania.