Rwanda kuwa na asilimia 50 ya wanawake mawaziri
19 Oktoba 2018Rwanda imetangaza wizani wa usawa wa jinsia kwa kuwa na asilimia 50 ya wanawake katika baraza la mawaziri. wanawake watakuwa nusu ya wajumbe 26 wa baraza la mawaziri la taifa hilo la Afrika Mashariki kutangaza azma hiyo ya kuongeza idadi ya wanawake katika baraza hilo lililopunguzwa na kusalia na mawaziri 26.
Rwanda imetangaza nia hiyo siku mbili baada ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kutangaza asilimia 50 ya wanawake kwenye baraza lake la mawaziri na kuwa moja ya mabaraza machache duniani yenye idadi hiyo.
Rwanda sasa inakuwa miongoni mwa mataifa hayo machache, na mengi kati yao yakiwa barani Ulaya ambako asilimia 50 ama zaidi ya mawaziri ni wanawake, hii ikiwa ni kulingana na Muungano wa mabunge na taasisi ya wanawake ya Umoja wa Mataifa .
Taifa hilo linatambuliwa kimataifa kutokana na uwakilishi wa wanawake serikalini, unaofikia asilimia 61 ya wabunge.