1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rushwa yatishia hatua za kukabiliana na hali ya hewa

11 Februari 2025

Ripoti ya Shirika la Transparency International imeonya kwamba rushwa inatishia juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

https://p.dw.com/p/4qIad
Transparency International
Shirika la Transparency International limependekeza pia kuondoa mianya inayowezesha ushawishi usiofaa katika mchakato wa kuunda sera ya hali ya hewa.Picha: Rafael Henrique/ZUMA Wire/IMAGO

Kulingana na ripoti hiyo inayoangazia rushwa Kimataifa, rushwa inazuia hatua madhubuti katika masuala ya hali ya hewa kwa kuzuia kupitishwa kwa sera kabambe.

Ripoti ya shirika hilo ya 2024 inalenga, "Kielelezo cha Muelekeo wa Rushwa" inaonyesha kuwa nchi nyingi, ziwe zinakabiliana na ongezeko la joto au zimeandaa mikutano ya Umoja wa Mataifa ya hali ya hewa, zina alama duni kuliko hapo awali.

Soma pia: Hizi ndizo nchi zenye ufisadi mdogo zaidi duniani

Kwa mfano, Brazili, ambayo ni mwenyeji wa mazungumzo ya hali ya hewa ya COP30 mwaka huu, ilipata alama 34, alama yake ya chini kuwahi kutokea - ikiashiria kiwango cha juu cha rushwa.

Akizungumzia matokeo ya ripoti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Transparency International Maira Martini amesema wanaohusika na rushwa sio tu wanaunda lakini mara nyingi huamuru sera na kuvunja mustakabali wa ukaguzi.

Azerbaijan, ambayo ilikuwa mwenyeji wa mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa mwaka jana, ilipata alama 22 pekee.

Soma pia: Rushwa yachangia mgogoro wa kidemokrasia duniani

Huku nchi nyingi tajiri ambazo hapo awali zimechukua jukumu kuu katika mazungumzo ya hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na Kanada, Marekani na New Zealand, pia zikitajwa kuwa ongezeko la rushwa.

Ufisadi katika sekta ya umma

Nembo ya Shirika la Transparency International
Ripoti ya Transparency International iligundua kuwa nchi 47 kati ya 180 zilizofanyiwa utafiti zilikuwa na ongezeko la visa vya rushwa.Picha: Soeren Stache/picture alliance/dpa

Ripoti hiyo ya kila mwaka inayapa mataifa yaliyo na hatari kubwa zaidi ya ufisadi hasa katika sekta ya umma alama ya chini kutoka sifuri hadi 100.

Nchi zilizotajwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha rushwa ni zile zilizokumbwa na migogoro, kama vile Sudan, Venezuela, Somalia, Syria, Eritrea na Yemen. Sudan Kusini ilishuka hadi mwisho wa orodha, huku Denmark ikiwa na viwango bora zaidi.

Ripoti hiyo pia iligundua kuwa nchi 47 kati ya 180 zilizofanyiwa utafiti zilikuwa na ongezeko la visa vya rushwa tangu shirika hilo lilipoanza kutumia mbinu yake ya sasa kwa nafasi yake ya kimataifa mwaka 2012. Nchi hizo ni pamoja na Ujerumani, Austria, Brazil, Ufaransa, Haiti na Hungary.

Soma pia: Ujerumani bado ina kazi kubwa ya kupambana na Ufisadi

Shirika hilo limetoa mapendekezo kadhaa katika kukabiliana na ongezeko hilo ikiwa ni pamoja na uadilifu na kupambana na rushwa katika masuala ya fedha na hatua za hali ya hewa. Kuimarisha uchunguzi, ulinzi na vikwazo ili kukabiliana na rushwa inayohusiana na uhalifu wa mazingira.

Soma pia: TI: Rushwa imeongezeka Afrika

Imependekeza pia kuondoa mianya inayowezesha ushawishi usiofaa katika mchakato wa kuunda sera ya hali ya hewa, katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa.

//https://p.dw.com/p/4qHxw
//https://www.transparency.org/en/news/how-corruption-undermines-global-climate-efforts