1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK:Rais Bush ziarani Ujerumani Mashariki

12 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8K

.

Rais Gorge Bush wa Marekani atawasili baadae leo katika jimbo la Rostock mashariki mwa Ujerumani kwa ziara rasmi nchini humu.

Rais Bush amepangiwa kuwa na mazungumzo na kansela Angela Merkel wa Ujerumani hapo kesho mazungumzo ambayo yanatarajiwa kutuwama juu ya mgogoro wa Nuklia wa Iran na mpango wa makombora ya Korea Kaskazini.Usalama umeimarishwa huko Rostock ambapo polisi 12 elfu wamewekwa kulinda usalama wakati wa ziara ya rais Bush.

Baada ya kukamilisha ziara yake rais Bush ataelekea nchini Urussi ijumaa kukutana na viongozi wa mataifa tajiri kiviwanda duniani kwenye mkutano wa kilele wa G8 huko St Petersburg.