1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Papa mpya ameisifu kazi ya waandishi wa habari

23 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFK9

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amewashukuru waandishi wa habari kwa kazi waliyoitekeleza kuripoti uchaguzi wa kihistoria wa Papa mpya.Akizungumza kwa lugha nne mbali mbali,Baba Mtakatifu alisema vyombo vya habari viliwapa Wakatoliki kote duniani nafasi ya kushuhudia matokeo hayo.Mkutano wa hii leo pamoja na waandishi wa habari mia kadhaa ni mkutano wa kwanza wa Papa mpya pamoja na watu walio nje ya Vatikan.Hiyo kesho kiasi ya kama watu nusu milioni wanatazamiwa kumiminika kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro kumuona Kadinali wa zamani Joseph Ratzinger,mzaliwa wa Ujerumani,akisheherekea misa ya kutawazwa Baba Mtakatifu.Siku ya jumapili hadi Wajerumani laki moja pia wanatarajiwa mjini Rome.Kansela Gerhard Schroeder na Rais Horst Köhler wa Ujerumani wataungana na viongozi wengine wa kimataifa mjini Rome kwenye sherehe ya hiyo kesho.