1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIADHA: Mkenyan Kipkosgei ashinda Ufaransa

19 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFht
Mwanariadha wa Kenya Luke KIPKOSGEI aliondoka na ushindi wa mashindano ya mbio za nyika yaliofanyika jumapili katika mji wa magharibi mwa Ufaransa wa Le Mans. KIPKOSGEI alitimka mbio hizo za cross-country za 10,6 km dakika 31 na nukta 19 akifuatiwa na Mkenya mwengine Julius KIPTOO pamoja na Mfaransa Driss El-HIMER. Nafasi ya 4 ilishikwa na George MURARA wa Kenya akimtangulia Martin SULLE wa Tanzania. Kwa wanawake, ushindi ulimwendea pia Mkenya Rahab NDUNGU, aliyekimbia 5,5 km mnamo 18:03 akiwatangulia Dirbe ALEMU wa Ethiopia na Fatima YVELAIN wa Ufaransa.