1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Republican wambwaga mshirika wa Trump nafasi ya spika

21 Oktoba 2023

Wabunge wa chama cha Republican nchini Marekani, kwa mara nyingine wameshindwa kumchagua spika wa bunge. Wanachama 25 kutoka Republican waliungana na Wademocrat kupiga kura ya kukataa azma ya Jordan kuwania uspika.

https://p.dw.com/p/4Xq7Q
USA Jim Jordan Kongressprecher
Picha: J. Scott Applewhite/AP Photo/picture alliance

Wabunge wa chama cha Republican nchini Marekani, kwa mara nyingine wameshindwa kumchagua spika wa bunge. Hatua hiyo ni baada ya mhafidhina Jim Jordan kupoteza kura ya siri ambayo ingemwezesha kusalia kama mgombea wa chama cha Republican katika nafasi ya spika. Marekani: hama cha Republican chashindwa kuusuluhisha mgawanyiko ndani ya chama hicho

Wanachama 25 kutoka Republican waliungana na Wademocrat kupiga kura ya kukataa azma ya Jordan kuwania uspika, hiyo ikiwa ni mara ya tatu ndani ya siku nne. Mwanasiasa huyo anaungwa mkono na Rais wa zamani Donald Trump.

Tangu Kevin McCarthy alivyong'olewa katika kiti cha Uspika siku 17 zilizopita, hakuna mgombea ambaye amekusanya kura zinazohitajika kuweza kuchukua mikoba yake. Rais Joe Biden amewasilisha ombi la msaada wa dola bilioni 100 za ufadhili wa kijeshi kwa Ukraine na Israel, lakini hakuna kinachoweza kuidhinishwa hadi spika atakapochaguliwa.