1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramos aurefusha mkataba wake katika Real Madrid

17 Agosti 2015

Beki wa Real Madrid Sergio Ramos ameurefusha mkataba wake katika klabu hiyo ya La Liga hadi mwaka wa 2020, hivyo kukamilisha uvumi kuwa huenda akajiunga na timu ya Ligi ya Premier ya England, Manchester United

https://p.dw.com/p/1GGkh
FIFA Klub-WM Real Madrid gegen San Lorenzo
Picha: Reuters/Boudlal

Ramos mwenye umri wa miaka 29, amesema amefurahi kusaini mkataba huo mpya ili kuichezea Real kwa misimu mitano ijayo. Inaripotiwa kuwa Mhispania huyo amepewa nyongeza kubwa ya mshahara isipokuwa maelezo ya kifedha ya mkataba huo hayajatolewa. Ramos amesema “kichwa changu na moyo wangu kila mara vimekuwa katika klabu hii, ijapokuwa mazungumzo ya kuurefusha mkataba wangu yamechukua muda mrefu“. Amesema hajawahi kusema kuwa anataka kuondoka na kuwa angetaka kustaafu katika klabu hiyo.

Ramos alijiunga na Real Madrid kutoka Sevilla mwaka wa 2005 na ameisaidia kushinda Taji la Champions League na mataji matatu ya ligi ya Uhispania. Ramos alichukua unahodha wa timu hiyo kutoka kwa mlinda mlango wa muda mrefu Iker Casillas alyejiunga na Porto. Wakati huo huo Real Madrid inakaribia kumsaini kiungo Mateo Kovacic kutoka Inter Milan.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Sessanga