1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Ramaphosa akabiliwa na mjadala wa kumuondoa madarakani

13 Desemba 2022

Bunge la Afrika Kusini linatarajiwa kujadili ikiwa litaanzisha mchakato wa kuamua ikiwa Rais Cyril Ramaphosa anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi ataondolewa madarakani au la.

https://p.dw.com/p/4Krf0
UK, London | Cyril Ramaphosa Präsident von Südafrika
Picha: Wiktor Szymanowicz/AA/picture alliance

Cyril Ramaphosa aliyetizamwa kama mpambanaji dhidi ya rushwa baada ya mtangulizi wake ambaye utawala wake ulizongwa na kashfa za ufisadi Jacob Zuma, pia anakabiliwa na madai ya kujaribu kuficha fedha nyingi za wizi.

Ripoti ya jopo huru la uchunguzi limesema huenda Ramaphosa ana hatia ya ukiukwaji mkubwa wa sheria na utovu wa nidhamu, na hayo yatakuwa miongoni mwa masuala ya kujadiliwa kwenye kikao cha bunge mjini Capetown.

Chama tawala cha ANC kinamuunga mkono Ramaphosa na kimetaka jumla ya wabunge wake 230 kwenye bunge lenye wajumbe 400 kupinga kuondolewa kwake.

Upinzani umeungana kuhusu suala hilo na haijulikani ikiwa baadhi ya wabunge wa ANC, chama ambacho kimegawika, wataungana na upinzani dhidi ya Ramaphosa.