RAMALLAH:Serikali mpya kuapishwa katika Palestina
17 Juni 2007Matangazo
Rais wa Mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas ametia saini agizo la kuunda baraza jipya la mawaziri.Afisa mmoja alie karibu na bwana Abbas amefahamisha hayo.Lakini chama cha Hamas kimesema kuwa hatua ya rais Abbas inaenda kinyume na sheria.
Habari zaidi zinasema kuwa mawaziri 11, wataalamu pamoja na waziri mkuu mpya bwana Salam Fayyad wanatarajiwa kuapishwa .