RAMALLAH:Baraza jipya la Usalama laundwa Palestina
15 Aprili 2007Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameunda baraza jipya la usalama wa kitaifa linaloshirikisha kwa mara ya kwanza vyama vya Hamas na Fatah.Baraza hilo linalolenga kudumisha usalama katika maeneo yanayokumbwa na ghasia na kuongozwa na Rais Abbas na Waziri Mkuu Ismail Hanniyeh.
Hii ni mara ya kwanza kwa chama cha Hamas kilicho mshiriki wa ngazi ya juu katika serikali ya kitaifa kupata nafasi kama hiyo.Baraza hilo linalenga kuwaleta pamoja majeshi ya usalama.
Kulingana na afisa wa serikali aliyezungumza na shirika la habari la AP Baraza hilo aidha linajumuisha mawaziri wa mambo ya ndani,mashauri ya kigeni vilevile sheria ili kupanga mikakati ya kisiasa na usalama.
Eneo la Ukanda wa Gaza linakumbwa na ghasia nyingi hata baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa mwezi jana inayolenga kumaliza mivutano inayokumba vyama vya Hamas na Fatah.