1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah: Wapalestina waunda baraza jipya la mawaziri

13 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDz
Rais Yasser Arafat jana alikula kiapo mbele ya baraza la mawaziri la Wapalestina ambalo lilisubiriwa muda mrefu, juu ya kuendelezwa mazungumzo ya amani yanayoungwa mkono na Marekani pamoja na Israel na Waziri Mkuu Ahmed Qurie alikula kiapo kujitafutia njia ya kusitisha mapigano. Akizungumza bnungeni, Arafat, ambaye mara kwa mara anaelezwa na Marekani kuwa kipengee cha amani, alitumia matamshi ya kujongeleana, ambayo ni nadra kusikilizwa na watu wake mnamo miaka mitatu ya machafuko. Lakini waziri wa ulinzi wa Israel Shaul Mofaz akizungumza mjini Washington, alisema itapita miaka mingi hadi kufikia mapatano ya kudumu pamoja na Wapalestina.