1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Wapalestina na kumbukumbu ya msiba mkuu

15 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFDO

Wapalestina leo wana kumbukumbu ya miaka 57 ya kile wanachokiona kuwa msiba mkuu wa kuanzishwa kwa taifa la Israel ambapo maandamano kadhaa yamepangwa kufanyika pamoja na kutolewa kwa hotuba katika siku hii ya Naqba.

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas ambaye hivi sasa yuko ziarani nchini Japani anatazamiwa kutuma ujumbe kwa njia ya kanda akisema kwamba siku hii ni mbaya kabisa katika historia ya wananchi wa Palestina.Pia anatarajiwa kusisitiza kwamba uhalifu huo katu hautosamehewa na Wapalestina.

Maandamano kadhaa yanatazamiwa kufanyika katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu na Israel ikiwa ni pamoja na mji wa Gaza ambapo maelfu ya watu wanatarajiwa kuandamana.

Wapalestina na Waarabu wa Israel wanaiona tarehe 15 mwezi wa Mei ni Siku ya Naqba ambapo mamia na maelfu ya Wapalestina walikimbia nyumba zao au walilazimishwa kuhama wakati wa kuundwa kwa taifa la Israel.