1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH. Wanamgambo wa kipalestina waapa kulipiza kisasi.

15 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMy

Kundi la wanamgambo wa kipalestina limeapa kulipiza kisasi kwa kuuwawa kwa mwanachama wake na wanajeshi wa Israel. Hata hivyo msemaji wa kundi hilo la wanamgambo wa Al Aqsa amesema uamuzi huo hautaathiri mkataba wa kusitisha mapigano uliafikiwa na pande hizo mbili. Mwanamgambo huyo alipigwa risasi na kuuwawa wakati wa uvamizi wa kambi ya wakimbizi karibu na mji wa Nablus huko ukingo wa magharibi. Duru za jehi la Israel zinasema wanajeshi wa Israel walimpiga risasi mwanamgambo huyo alipoanza kuwafyatulia risasi. Lakini wakaazi wa kambi hiyo wanasema wanajeshi hao ndio walioanza kufyatua risasi. Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas ameyalaani maujai hayo akiyataja kuwa ukiukaji wa mkataba wa kuyasitisha mapigano alioutangaza yeye pamoja na waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon mwezi Februari.