1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Rice asema suluhisho la kudumu lahitajiwa

25 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG46

Rais Mahmud Abbas wa Wapalestina ametoa mwito kwa kusitisha mapigano moja kwa moja nchini Lebanon na katika maeneo ya Kipalestina.Abbas alitoa mwito huo baada ya kukutana na waziri wa nje wa Marekani,Condoleezza Rice aliemtembelea.Rice kwa upande wake amesisitiza kuwa suluhisho la kudumu linahitajiwa ili kumaliza mgogoro kati ya Israel na Hezbollah.Akaongezea kuwa mzozo wa Gaza pia unapaswa kupatiwa suluhisho.Rice alikwenda Ukanda wa Magharibi kukutana na Abbas baada ya kuwa na mazungumzo pamoja na waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert mjini Jerusalem.