1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Naibu Wazizi Mkuu wa Palestina mbaroni Israel

20 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDK6

Wanajeshi wa Israel wanamshilikia Naibu Waziri Mkuu wa Palestina Nasser Shaer.

Mke wa mbunge huyo amesema wanajeshi walivamia nyumba yao mjini Ramallah na kumchukuwa kabla ya alfajiri. Amesema kwamba mume wake amekuwa mafichoni tokea Israel ilipoanza msako wake wa wanamgambo mwishoni mwa mwezi wa Juni baada ya wanamgambo wa Hamas kujipenyeza kusini mwa Israel na kumteka nyara mwanajeshi mmoja wa Israel.

Msemaji wa jeshi la Israel amethibitisha kwamba wanajeshi wamemchukuwa Shaer na kumweka mahabusu na kusema kwamba ni kutokana na kuwa mwanachama katika kundi la kigaidi.

Wanachama wanne wa baraza la mawaziri linaloongoza serikali ya Palestina na wabunge wake 28 wako katika mahabusu nchini Israel.