1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Mripuko wauwa 15 Gaza

24 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEYF

Takriban Wapalestina 15 wameuwawa na wengine 80 kujeruhiwa baada ya gari aina ya jeep kuripuka katika gwaride la kijeshi lililoandaliwa na Hamas kundi la itikadi kali la Kiislam.

Mripuko huo mkubwa kabisa umetokea kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabaliya wakati maelfu ya watu wakisheherekea kujitowa kwa Israel hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza.Kundi la Fatah la kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas limesema katika taarifa kwamba Hamas inawajibika na kuuwawa kwa Wapalestina hao kwa vile walikuwa tayari wamekubaliana kwamba magwaride hayo ya kijeshi ni ya hatari kwa watu na yanapaswa kukomeshwa.

Hamas imesema mripuko huo ni matokeo ya shambulio la anga la Israel wakati Israel yenyewe imekanusha kuhusika.

Wakati huo huo Waisrael watano wamejeruhiwa wakati wanamgambo wa Kipalestina walipofyetuwa roketi ndani ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza usiku wa kuamkia leo.