1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Kuahirishwa uchaguzi kwachemsha hasira

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF70

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas hapo jana ameahirisha uchaguzi wa bunge uliokuwa umepangwa kufanyika hao tarehe 17 mwezi wa July na hiyo kuzusha hasira kutoka kundi la siasa kali la Kiislam la Hamas ambalo lilikuwa likitarajia kujipatia ushindi mkubwa katika uchaguzi huo.

Taarifa ya Mamlaka ya Palestina imesema Abbas ameamua kufuta agizo la awali lililoweka tarehe 17 July kuwa siku ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo tarehe mpya itawekwa na agizo baada ya mashauriano na makundi tafauti ya Wapalestina na kupitishwa kwa sheria mpya ya uchaguzi na bunge la Palestina.

Uamuzi huo pia umechemsha hasira miongoni mwa wabunge akiwemo naibu spika Hassan Khreishe aliyetishia kujiuzulu kupinga uamuzi huo.