1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH-Kamanda mpya wa usalama wa ndaini wa Palestina ateuliwa.

27 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJ0

Maofisa wa Palestina wamesema kuwa Rais wa Mamlaka ya Wapalestina,Mahmoud Abbas,amemteua afisa mpya atakayesimamia usalama wa ndani wa Palestina,ambaye alisaidia kufanikisha kuchukuliwa kwa hatua kali za nidhamu kwa vikundi vya wanamgambo wa Kiislamu katika miaka ya 1990.

Uteuzi wa Rashid Abu Shbak kuwa mkuu mpya wa kikosi cha usalama,umezidi kuimarisha nafasi ya Rais Abbas,baada ya kutimuliwa maofisa wa ngazi ya juu waliokuwa wafuasi wa marehemu Yasser Arafat.

Waziri wa Ulinzi wa Israel,Shaul Mofaz amesema Rais Abbas amechukua hatua sahihi,lakini amemtaka kufanikisha matokeo zaidi na ya haraka.Mofaz ameongeza kusema kuwa pamoja na hayo,ni muhimu kwa hivi sasa kutoa nafasi kwa mchakato wa amani.