1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Hamas bado yagoma kuitambua Israel

23 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9s

Kundi la siasa kali la Hamas limesema litafuta mipango ya kuunda serikali ya Palestina ya umoja wa kitaifa iwapo kutawekwa masharti ya kulitambua taifa la Israel.

Tangazo hilo limetolewa na mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh.Awali Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amewaambia viongozi wa dunia katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba serikali yoyote ya umoja wa kitaifa itatambuwa haki ya kuwepo kwa taifa la Israel na kukanusha matumizi ya nguvu.

Abbas ameongeza kusema kwamba serikali hiyo ijayo itapigania kuundwa kwa taifa la Palestina pembezoni mwa Israel na kwamba pia itaheshimu makubaliano yote yalioko yaliofikiwa na taifa hilo la Kiyahudi miaka iliopita ikiwa ni pamoja na mkataba wa kutambuwana uliotiwa saini mjini Oslo Norway hapo mwaka 1993.