1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Blair ataka serikali ya umoja ya Palestina ipokelewe

10 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDe

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema leo hii kwamba dunia inapaswa kuikaribisha serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina kufuatia kususiwa kulikoleta madhara makubwa kwa serikali ya hivi sasa inayoongozwa na Hamas.

Blair ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kufutia mkutano wake na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina kwamba iwapo serikali hiyo itaundwa anaamini ni sahihi kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana na serikali hiyo.

Ziara ya Blair huko Ramallah ni mfululizo wa ziara yake Mashariki ya Kati yenye lengo la kuufufuwa mpango wa amani Mashariki ya Kati unaojulikana kama ramani ya amani.

Wakati huo huo Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema yuko tayari kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert bila ya masharti yoyote yale.Waziri Mkuu wa Israel alitowa kauli kama hiyo hapo jana.