1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Baraza la mawaziri la Hamas lajiuzulu.

14 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCU

Baraza la mawaziri lililokuwa likiongozwa na chama cha Hamas limejiuzulu kwa pamoja, kabla ya matarajio ya kuundwa kwa serikali mpya ya umoja wa kitaifa pamoja na chama kinachofuata msimamo wa kati cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas.

Msemaji wa baraza la mawaziri amesema kuwa mawaziri wote katika baraza hilo linaloongozwa na chama cha Hamas wamerejesha nyadhifa zao kwa waziri mkuu Ismail Haniyah.

Chama cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas cha Fatah kimekubali kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na chama chenye msimamo mkali cha Hamas katika juhudi za kuiondoa mamkala hiyo ya Wapalestina kutoka katika miezi kadha ya kutengwa kimataifa.