1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Abbas amewateua wakuu wapya wa usalama

24 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFK0

Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina amewateua makamanda wapya 3 wa usalama.Hiyo ni sehemu ya mageuzi makuu yanayotaraji kuwastaafisha kiasi ya maafisa 1,000 wa usalama.Vikosi vya usalama vimekosolewa na serikali za kigeni na Wapalestina wa kawaida kuhusika na ufisadi na uzembe na mara kwa mara kumetolewa wito wa kufanywa mageuzi.Miongoni mwa mabadiliko yaliofanywa nafasi ya Moussa Arafat,ambae ni binamu wa marehemu Yasser Arafat itachukuliwa na mwengine kama kamanda wa majeshi ya usalama wa taifa.