1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Zanzibar aunda kikosi kazi kuendeleza demokrasia

Salma Said10 Oktoba 2022

Daktari Hussein Ali Mwinyi azindua kikosi kazi maalumu cha kukusanya maoni ya wadau kuhusiana na hali ya kisiasa kwa upande wa Zanzibar.

https://p.dw.com/p/4I0HO
Tansania | Swahili International Day
Picha: Salma Said/DW

Jumla ya wajumbe 11 wameteuliwa katika kikosi hicho wakitokea kwenye vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wasomi

Mwenyekiti wa kikosi hicho ni Dk Ali Uki, Makamo Mwenyekiti ni Balozi Amina Salum Ali, wajumbe ni ACT Wazalendo Ismail Jussa, CCM Vuai Ali Vuai, Chadema Said Issa Mohammed, CUF Rukia Kassim Ahmed, Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir, mashirika yasiyo ya kiserikali Joseph Abdallah Meza, Taasisi za kidini, Sheikh Thabit Nauman Jongo na Padri Stanley Nikolas Nchinga, Mjumbe na Kutoka wasomi Mohammed Professa Mohammed Makame Haji Katibu ni Mohamme Ali Abdallah.

Akitoa neno fupi mbele ya Rais Msajili wa vyama vya kisiasa Jaji Fransic Mutungi ameahidi ofisi yake kufanyia kazi mapendekezo ili nchi ibaki salama.

Jumla ya hadidu rejea sita zimepewa kikosi kazi hicho kwa ajili ya kuzifanyia kazi kabla ya kuwasilisha ripoti hiyo kwa Rais wa Zanzibar kwa muda wa siku 14.

Akisoma hadidu rejea za kikosi kazi hicho mbele ya wajumbe  Katibu Mkuu ofisi ya makamo wa pili wa Rais Thabit Idarous Faina aliwaambia wajumbe kuwa hutuba za viongozi wakuu za ufunguaji na ufungaji wa mkutano wa wadau uliofanyika wiki iliyopita zihusishwe katika kazi hiyo.

Kazi kubwa walionayo ni kuchambua maoni yaliotolewa na wadau wa vyama vya siasa, asasi za kiraia pamoja wananchi kuhusiana na hali ya kisiasa nchini.