1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi arejea wito wa suluhisho la madola mawili mzozo wa Gaza

30 Mei 2024

Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito kwa mara nyingine wa kuundwa kwa taifa huru la Palestina na kuahidi kutuma msaada kwa umma Gaza, ambao unakabiliwa na hali mbaya ya kibinaadamu kutokana na vita vinavyoendelea.

https://p.dw.com/p/4gRyq
Rais Xi Jingping wa China na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.
Rais Xi Jingping wa China na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.Picha: Royal Court of Saudi Arabia/AA/picture alliance

Xi alikuwa akizungumza kwenye mkutano kati ya China na viongozi wa mataifa ya kiarabu unaofanyika leo mjini Beijing. 

Soma pia:Vifaru vya kijeshi vya Israel vyaendeleza mashambulizi Rafah

Amesema tangu Oktoba mwaka jana mzozo kati ya Israel na Palestina umetanuka na kuwatumbukiza watu kwenye masaibu ya kutisha. 

“Vita haviwezi kuendelea bila kikomo. Haki haiwezi kukosekana daima. Na iwapo kuna nia, shabaha ya kupatikana suluhu kwa kuundwa madola mawili haiwezi kudhoofishwa" Alisema Xi.

Kwenye mkutano huo wa mjini Beijing unaohudhuriwa na viongozi wa Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Tunisia, Rais Xi ameahidi kwamba nchi yake itatoa mchango wa angalau dola milioni 72 kusaidia utoaji misaada kwa ajili ya Ukanda wa Gaza.