1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMauritania

Rais wa zamani wa Mauritania kufikishwa mahakamani

24 Januari 2023

Kesi ya rushwa dhidi ya Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz inaanza kesho. Itakuwa ni tukio la nadra kiongozi wa zamani wa nchi barani Afrika kufikishwa mahakamani.

https://p.dw.com/p/4Mdjq
Symbolbild Mauretanische Junta-Mitglieder und EU
Picha: DW / DPA

Abdel Aziz, jenerali wa zamani mwenye umri wa miaka 66, anakabiliwa na mashitaka ya kujikusanyia mali kinyume cha sheria wakati wa utawala wake wa miaka 11.

Baada ya kuingia madarakani kupitia mapinduzi, alijiuzulu mwaka wa 2019 baada ya mihula miwili ya urais ambapo aliuangamiza uasi wa itikadi kali uliokuwa unatishia taifa hilo la Afrika Magharibi.

Abdel Aziz na vigogo wengine 11 kutoka utawala wake wa zamani walishitakiwa kwa tuhuma za rushwa, utakatishaji fedha na kujikusanyia mali kinyume cha sheria.

Washitakiwa wanajumuisha mmoja wa wakwe zake, mawaziri wakuu wawili wa zamani na mawawiri kadhaa wa zamani na wafanyabiashara. Rais huyo wa zamani anakataa kujibu maswali kuhusu chanzo cha utajiri wake.