1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron asema anazungumza na Bazoum kila siku

2 Septemba 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amesema jana kwamba amekuwa akifanya mazungumzo kila siku na rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum na kusisitiza kwa mara nyingine kwamba Ufaransa inamuunga mkono Bazoum.

https://p.dw.com/p/4VsBn
Kiongozi wa kijeshi nchini Niger Jenerali Abdourahmane Tiani akiwasili mjini Niamey kwa mkutano na mawaziri
Kiongozi wa kijeshi nchini Niger Jenerali Abdourahmane TianiPicha: Balima Boureima/Reuters

Macron amesema hawatambui viongozi wa kijeshi nchini humo na kwamba maamuzi yoyote yatakayofanywa na Ufaransa yatazingatia mazungumzo na Bazoum.

Matamshi hayo ya Rais Macron yalichapishwa katika mtandao wa kijamii wa ikulu ya Elysee ambapo alikuwa akizungumza na wanahabari Kusini mwa Ufaransa kuhusu masuala ya elimu.
 

Ufaransa yashutumiwa kwa kuingilia masuala ya ndani ya Niger

Katika hatua nyingine, viongozi wa kijeshi nchini Niger, wameishtumu Ufaransa kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo baada ya rais Macron kusisitiza kumuunga mkono Bazoum.
Soma pia:Burkina Faso yaidhinisha muswaada wa kutuma kikosi Niger

Uongozi huo wa kijeshi umesema hayo kupitia taarifa iliyotolewa kupitia televisheni ya taifa na msemaji wake kanali Amadou Abdramane.