1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi afariki dunia

Angela Mdungu
25 Julai 2019

Rais wa  Tunisia  Beji Caid Essebsi  amefariki  dunia  katika hospitali  ya  kijeshi mjini  Tunis

https://p.dw.com/p/3MiGk
Frankreich Paris | Tunesiens Präsident Beji Caid Essebsi
Picha: picture-alliance/abacapres/S. Lemouton

Taarifa  za  kifo  chake zimetolewa  kupitia  ukurasa wa  facebook kwa  lugha  ya  Kiarabu na  kwamba amefariki  asubuhi  ya  leo. Essebsi  alipelekwa  katika hospitali  ya  jeshi  jana jioni kwa  mara  ya  pili  katika muda  wa  karibu  mwezi mmoja.

Essebsi  mwenye  umri wa  miaka  92, amekuwa  madarakani  tangu  mwishoni mwa  2014.

Amejitokeza  mara  chache  hadharani  tangu  wakati  huo na  alitia  saini amri ya  rais  kuanzisha mchakato  wa uchaguzi  wa  bunge  na  rais  nchini  humo uliopangwa kufanyika  baadaye mwaka  huu.