1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuwania muhula wa nne madarakani

20 Septemba 2023

Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa mara ya kwanza amesema, ana mpango wa kugombea kwa awamu ya nne katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwakani.

https://p.dw.com/p/4Wawk
Paul Kagame amekuwa rais wa Rwanda tangu mwaka 2000.
Paul Kagame amekuwa rais wa Rwanda tangu mwaka 2000.Picha: Presse- und Kommunikationsdienst der Präsidentschaft der DR Kongo

Kagame aliyetawala taifa hilo kwa mkono wa chuma na kwa miongo kadhaa ameliambia gazeti la lugha ya kifaransa la Jeune Afrique kuhusiana na nia yake hiyo katika mahojiano yaliyochapishwa mitandaoni jana Jumanne.

Amesema anafurahishwa na imani waliyonayo watu wa Rwanda juu yake na kuahidi kuwatumikia siku zote na kwa namna atakavyoweza.

Kagame hajawahi kuweka wazi nia ya kuwania tena urais, lakini mabadiliko tata ya katiba yalimfungulia njia ya kuwania awamu ya tatu na kushinda kwa asilimia 99 katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2017.

Soma pia:

Rais Kagame afanya mabadiliko katika idara ya jeshi