1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini yaiita Japan "mshirika" kwenye Siku ya Ukombozi

15 Agosti 2023

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol hii leo ameitaja Japan, ambayo ni mkoloni wa zamani wa taifa lake, kuwa "mshirika" mwenye maadili na maslahi yanayofanana

https://p.dw.com/p/4VBG8
Südkorea Präsident Yoon Suk-yeol
Picha: Foto Olimpik/NurPhoto/IMAGO

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol hii leo ameitaja Japan, ambayo ni mkoloni wa zamani wa taifa lake, kuwa "mshirika" mwenye maadili na maslahi yanayofanana katika wakati anatafuta kuimarisha mahusiano na utawala mjini Tokyo chini ya kitisho kinachoongeza kutoka Korea Kaskazini.

Soma pia: Waziri mkuu wa Japan aonesha huruma juu ya ukoloni wa nchi yake nchini Korea Kusini

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha ukombozi wa rasi ya Korea kutoka utawala wa kikoloni wa Japan, rais Yoon amesema hivi sasa mataifa hayo mawili ni washirika wakutumainiana.

"Ili kuvikabili vitisho vya nyuklia vya Korea Kaskazini, Japan, Marekani na Korea Kusini ni lazima zisishirikiane kwa karibu kwenye maeneo ya ujasusi na kubadilisha taarifa kwa wakati kuhusu silaha za nyuklia za Korea Kaskazini na makombora yake ya masafa".

Korea Kusini na Japan, ambazo ni washirika wakubwa wa Marekani, zimekuwa kwenye misuguano juu ya masuala ya kihistoria yanayofungaamnishwa na utawala katili wa Japan iliyoikalia kwa mabavu rasi ya Korea kati ya mwaka 1910 hadi 1945.