1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Afrika Kusini atuma pole kwa watu wa Namibia

4 Februari 2024

Viongozi mbalimbali barani Afrika wanaendelea kutuma salamu za pole kwa Namibia baada ya kifo cha rais Hage Geingob aliyefariki leo akiwa na umri wa miaka 82.

https://p.dw.com/p/4c1oO
USA New York 2023 | Namibias Präsident Hage Geingob spricht bei der UN-Generalversammlung
Picha: Caitlin Ochs/REUTERS

Viongozi mbalimbali barani Afrika wanaendelea kutuma salamu za pole kwa Namibia baada ya kifo cha rais Hage Geingob aliyefariki leo akiwa na umri wa miaka 82.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amesema: "Afrika Kusini inaungana na watu wa Namibia kuomboleza kifo cha kiongozi, mzalendo na rafiki wa Afrika Kusini. Ramaphosa amesema Rais Geingob alikuwa mwanajeshi mkongwe wa ukombozi wa Namibia kutoka kwa wakoloni na wabaguzi wa rangi.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia mtandao wa X zamani Twitter amesema kwamba, amehuzunishwa na kifo cha rais Geingob akimtaja kama rafiki mkubwa wa Tanzania, wakati rais Willium Ruto wa Kenya akimtaja Geingob aliamini katika Afrika ilioungana.

Kabla ya kuwa rais Geingob alikuwa Waziri Mkuu wa Namibia mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake ambapo alihudumu kwenye wadhfa huo kwa muda mrefu. Alikuwa kinara wa kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya kugeuka na kuwa mwanasiasa.