1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Putin atishia kushambulia magharibi kupitia mataifa mengine

6 Juni 2024

Rais Valdimir Putin ameonya jana Jumatano kwamba Urusi inaweza ikawapatia mataifa mengine makombora ya masafa marefu kwa ajili ya kushambulia maeneo lengwa kwenye mataifa ya magharibi.

https://p.dw.com/p/4ghtP
Urusi yatishia kuishambulia magharibi kupitia mataifa mengine
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu wakiondoka kwenye bustani ya Red Square baada ya gwaride la kijeshi la Siku ya Ushindi huko Moscow, Urusi, Mei 9, 2024,Picha: Alexander Zemlianichenko/AP Photo/picture alliance

Hatua hii amesema itakuwa ni jibu ya ruhusa iliyotolewa na washirika wa jumuiya ya NATO kwa Ukraine kutumia silaha inazopewa na magharibi kuishambulia Urusi.

Putin aidha amethibitisha kwa mara nyingine kuhusu utayari wa kutumia sialaha za nyuklia ikiwa kutakuwa na kitisho chochote kwenye eneo lake.

Amesema hatua hiyo ya magharibi itazidi kudhoofisha usalama wa kimataifa na kuchochea matatizo makubwa, na itaashiria wazi ushiriki wake wa moja kwa moja kwenye vita kati ya Urusi na Ukraine na kuongeza kuwa wana haki ya kuchukua hatua kama hiyo.

Putin alikuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo vya magharibi, jambo ambalo analifanya kwa nadra mno tangu alipoivamia Ukraine.