1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia awa mgombea urais wa CCM

20 Januari 2025

Rais Samia awa mgombea wa urais wa CCM

https://p.dw.com/p/4pMTf
Tansania Kamala Harris  Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano na waandishi wa habari.Picha: Ericky Boniphace/AP/picture alliance

Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana Jumapili kimemteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba kwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Rais Samia aliingia madarakani mwaka 2021 baada ya kifo cha ghafla cha mtangulizi wake John Pombe Magufuli.

Chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilifanya mkutano mkuu mwishoni mwa juma ambapo kilihitimisha kwa kimemtaja kuwa yeye ndiye atakuwa mgombea pekee kwa kuwania urais wa taifa hilo kwa chama hicho katika uchaguzi wa Oktoba.

Ukosoaji wa jumuiya ya kimataifa kwa mamlaka ya Tanzania

Baada ya kushika madaraka, katika siku za mwanzo Hassan alisifiwa kwa kulegeza vikwazo ambavyo Magufuli aliuwekea upinzani na vyombo vya habari kwa taifa hilo lenye takriban watu milioni 67. Lakini baadae makundi ya haki za binadamu na mataifa ya Magharibi wamekuwa wakikosoa kwa kile wanachokiona kama kuanza upya kwa ukandamizaji. Wanasiasa wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema wamekamatwa na viongozi kadhaa wa upinzani kutekwa na kuuawa.

Katika hotiba yake ya kuhitimisha mkutano huo Rais Samia Suluhu Hassan amesikika akisema "Tumefanikiwa kwa mambo mengi katika miaka minne iliyopita na ninaahidi kufanya mengi zaidi katika muhula ujao." na kuongoza kuwa "Nawaomba wote kudumisha umoja wetu tunapoelekea kwenye uchaguzi."

Dokta Emmanuel Nchimbi ateuliwa kuwa mgombea mwenza

Rais huyo ambae ni kwa mara ya kwanza kushiriki mchakato wa kugombea urais kwa kwenda kupigiwa kura ameonya kuwa uchaguzi unaweza kuwagawanya kwa kiwango kikubwa lakini anaamini wataweza kudumisha umoja na tayari wana wagombea.

 Tansania | Generalsekretär der Regierungspartei in Tansania CCM Emmanuel John Nchimbi
Katibu Mkuu wa Chama Tawala Tanzania CCM Emmanuel John Nchimbi na sasa mgombea mwenza kwa uchaguzi wa 2025.Picha: CCM

Aidha Rais Samia amemteua Katibu Mkuu wa CCM, Dokta Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi huo. Endapo chama hicho kitafanikiwa kuchukua dola Nchimbi atakuwa makamu wa rais wa taifa hilo.

Wiki iliyopita, kiongozi wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo), Dorothy Semu, alitangaza nia ya kuwania urais kwa kumpa changamoto Rais Samia katika uchaguzi huo wa mwezi Oktoba.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) bado hakijaanza mchakato wa kumchagua mgombea wake, lakini kinatarajiwa kumchagua mwenyekiti wake mpya siku ya Jumanne.

Soma zaidi: Chama cha CCM chapata Makamu Mwenyekiti mpya

Hata hivyo, mwishoni mwa mwaka jana chama hicho kilionya kuwa kinakusudia kususia uchaguzi wa 2025 ikiwa mageuzi makubwa ya mfumo wa uchaguzi hayatatekelezwa. Hitaji hilo la muda mrefu limepuuzwa mara kwa mara na chama tawala CCM.

Chanzo: AFP