Rais mteule Daniel Chapo ameapishwa kuiongoza Msumbiji
15 Januari 2025Matangazo
Chapo ameapishwa baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba mwaka jana.Miongoni mwa viongozi wa kigeni waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na rais wa Afrika Kusini,Cyril Ramaphosa.
Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane anayepinga matokeo hayo, amesema wafuasi wake watasimamisha shughuli zote katika taifa hilo kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo anasema yamempokonya ushindi.
Soma pia: Msumbiji yawapisha wabunge wapya kukiwa na hali ya utulivu
Jana, Mondlane alisema yuko tayari kuilemaza nchi kwa muhula wote wa uongozi wa Chapo na kwamba atapambana pia mahakamani. Rais mteule Daniel Chapo, mwenye umri wa miaka 48 aliyewahi kuwa Gavana,- atamrithi Rais Filipe Nyusi aliyemaliza muda wake.