Rais mpya wa Georgia Mikheil Kavelashvili aapishwa
29 Desemba 2024Rais anayeondoka madarakani Salome Zourabichvili, ambaye anaiunga mkono Umoja wa Ulaya, amewaambia wafuasi wake kwamba anaondoka ikulu, lakini anasalia kuwa rais halali. Awali, Zourabichvili alisisitiza kuwa katu hataondoka madarakani.
Kwa wiki kadhaa, maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana kila siku nchini Georgia, wakitaka kurejeshwa kwa sera zinazounga mkono Umoja wa Ulaya.
Soma pia: Estonia yaongeza vikwazo dhidi ya viongozi wa Georgia
Aidha wamekuwa wakitaka uchaguzi wa bunge uliofanyika Oktoba, ambao chama cha kizalendo kinachotawala Georgian Dream party kilijitangaza mshindi, urudiwe.
Waandamanaji wana hofu kwamba chama hicho kina uhusiano wa karibu na Urusi na kitaimarisha urafiki huo, miongo kadhaa tangu ilipojitoa kwenye iliyokuwa muungano wa kisovieti.
Tayari chama tawala kimesimamisha mazungumzo ya nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya hadi mwaka 2028, na kusababisha maandamano kote Georgia.