1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia Uganda wanahofu ya kuenea virusi vya Corona nchini mwao

24 Aprili 2020

Raia wa Uganda wameingiwa na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 kutokana na shughuli za uchukuzi kati ya mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kufuatia waendeshaji kadhaa wa malori kugunduliwa kuwa na virusi vya Corona

https://p.dw.com/p/3bMSN
Coronavirus Uganda Kampala Temperaturmessung
Picha: AFP/S. Sadurni

Katika muda wa siku saba, madereva 16 wa magari ya mizigo wamegunduliwa kuwa na virusi vya corona. Hii ni baada ya kupimwa kwenye mipaka ya Busia, Malaba na Mutukula kwa upande wa Uganda. Idadi hii imechangia pakubwa kwa ile ya wagonjwa waliogunduliwa Uganda kufikia 74. Siku ya Alhamisi pekee, madereva 11, 6 kutoka Tanzania kwenye mpaka wa Mutukula na 5 kwenye mipaka ya Busia na Malaba.

Hiki ndicho chanzo cha hofu na mashaka miongoni mwa waganda kuhusu wimbi hilo wanaloelezea kuwa tishio baada ya juhudi za kudhibiti ugonjwa huo ndani ya nchi kuoenekana kuzaa matunda.

"Tunaogopa kwa ajili ukiona hapo awali hali ilikuwa si mbaya hapa Uganda kutokana na wagonjwa wachache wa Corona. Hawa ndugu zetu madereva tabia zao zi hatari wanaweza kuambukiza watu wengi, maambukizi haya ya madereva yanatisha mno na huenda . Hivi ndivyo COVID-19 itasambaa kwa haraka Afrika Mashariki," walisema baadhi ya wananchi.

Naye wakili na mtetezi wa haki za binadamu Gawaya Tegule anatahadharisha kuwa pana haja ya mataifa ya Afrika Mashariki kuwa na mikakati ya pamoja kukabliana na ugonjwa wa COVID-19.

"Huwezi kusema kwamba Uganda tuko vizuri kwa sababu wagonjwa ni wachache. Mtu atatoka Tanzania ataingia hapa Uganda na kuambuzi watu wengi," alisema Gawaya Tegule wakili na mtetezi wa haki za binaadamu.

Mjadala mkubwa waibuka kufuatia kuendelea kwa shughuli za uchukuzi wa mizigo

Pakistan LKW-Fahrer
Picha: picture-alliance/dpa/EPA/A. Gulfam

Suala la kuendelezwa kwa shughuli za uchukuzi wa mizigo kati ya mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki limeibua mjadala mkubwa katika ngazi za serikali, siasa na wafanyabiashara. Serikali imesisitiza kuwa shughuli za uchukuzi lazima ziendelee ndani, kutoka na kuingia nchini ili uchumi wa nchi usikwame katika kipindi hiki ambapo bidhaa nyingi zinahitajika kukidhi mahitaji ya watu walio chini ya karantini.

Waziri wa biashara wa Uganda Amelia Kyambadde amesema wamiliki wote wa mizigo wameagizwa kuwa na madereva mbadala iwapo mmoja atagunduliwa kuwa na COVID-19 mwingineataendelea na dafari.

Kwa upande wao waendeshaji na wafanyabiashara wanaoshirika katika uchukuzi wamefurahia juhudi zilizoanzishwa za kuwapima na kuendelea na safari zao huku matokeo yakitolewa baadaye.

Yule ambaye hugunduliwa kuwa na virusi hufuatwa popote alipo safarini na kushughulikiwa kimatibabu. "Kupimwa si vibaya tatizo ni chewesha kutupa matokeo yetu tuendee au tusiendelee na safari," alisema Bashir Yusuf mmoja kati ya madereva waliovuka kutoka Tanzania

Hata hivyo, kama ilivyo ada madereva hao wana jamaa na marafiki njiani ambao huwasimamisha. Rais Museveni ametoa onyo kali kwa watu hao hasa wanawake wajiepusha na tabia hiyo katika kipindi hiki. Wanawake watano waliokutana na mmoja kati ya wagonjwa hao alipokuwa safarini wamefuatiliwa na kuwekwa karantini.

Chanzo: Lubega Emmanuel DW Kampala