1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Wairan wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais

5 Julai 2024

Wairan wanapiga kura leo Ijumaa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais unaowakutanisha wagombea wawili walioshinda duru ya mwanzo iliyofanyika wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4huFQ
Iran | Uchaguzu
Kiongozi wa juu nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei akipiga kura yake kwenye uchaguzi wa rais mjini Tehran Julai 5, 2024Picha: Atta Kenare/AFP/Getty Images

Wagombea hao wawili ni mwanamageuzi Masoud Pezeshkian dhidi ya Saeed Jalili muhafidhina mwenye msimamo mkali.

Kiongozi wa juu zaidi nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei alipiga kura yake mapema asubuhi baada ya vituo vya kura kufunguliwa.

Duru ya mwanzo ya uchaguzi huo wa rais iliyofanyika wiki iliyopita ilimpa ushindi wa asilimia 42 Pezeshkian, mwanamageuzi pekee aliyeruhusiwa kugombea wakati mjumbe wa zamani wa Iran katika mazungumzo ya Nyuklia Saeed Jalili akinyakuwa nafasi ya pili kwa kupigiwa kura na asilimia 39 ya Wairan, kwa mujibu wa matokeo ya tume ya uchaguzi.

Asilimia 40 tu ya wapiga kura milioni 61 waliojiandikisha ndio waliojitokeza kwenye uchaguzi huo, idadi ndogo kabisa kuwahi kushuhudiwa katika uchaguzi wa rais nchini humo tangu mapinduzi ya kiislamu mwaka 1979.

Iran inafanya uchaguzi wa rais baada ya kifo cha Ebrahim rais,aliyekuwa rais wa nchi hiyo kilichotokana na ajali ya ndege.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW