1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Raia 7 wauawa kwenye shambulizi la jeshi la Sudan

15 Januari 2024

Wanaharakati nchini Sudan wamesema shambulizi la mabomu ya jeshi la Sudan yamewaua raia 7 siku ya Jumapii katika jimbo la White Nile.

https://p.dw.com/p/4bF0q
Mashambulizi katika jimbo la White Nile ni ishara ya hivi karibuni kwamba mapigano yanazidi kusambaa kuelekea upande wa kusini kutoka mji mkuu wa Khartoum.
Mashambulizi katika jimbo la White Nile ni ishara ya hivi karibuni kwamba mapigano yanazidi kusambaa kuelekea upande wa kusini kutoka mji mkuu wa Khartoum.Picha: AFP

Shambulizi hilo lililotokea kilometa 70 kusini mwa Khartoum, limeripotiwa na kundi moja la wanaharakati la kamati ya upinzani.

Makundi hayo ya upinzani wakati mmoja yaliwahi kuandaa maandamano ya kuunga mkono demokrasia, lakini sasa yanatoa msaada wakati wa vita.

Mashambulizi katika jimbo la White Nile ni ishara ya hivi karibuni kwamba mapigano yanazidi kusambaa kuelekea upande wa kusini kutoka mji mkuu wa Khartoum.

Katika jimbo linalopakana na Al-Jazira, maelfu ya wakimbizi wameyakimbia makazi yao tena, baada ya hapo awali kutafuta hifadhi kutoka Khartoum wakati wanamgambo wa RSF wakielekea kusini.

Umoja wa Mataifa ulisema Jumapili kuwa kupanuka kwa mapigano hayo katika mikoa iliyo muhimu kwa kilimo kumesababisha ongezeko kubwa la mahitaji ya kibinadamu wakati wa msimu wa mavuno.