1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT:Hispania kuwarejesha waafrika 70 nchini Morocco

7 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUB

Vyombo vya habari vya Morocco vimearifu kwamba watu sita kutoka mataifa ya Afrika wameuwawa katika mapambano na wanajeshi wa Morocco waliokuwa wakilinda uzio wa waya unaozunguka eneo la hispania la melilla.

Hii ni moja kati ya majaribio ya hivi karibuni yanayofanywa na na watu wanaotaka kuwa wahamiaji kinyume na sheria wanaojaribu kuingia eneo hilo la Melilla na eneo jingine la hispania lililoko katika pwani ya kaskazini ya Morocco ya Ceuta.

Wakati huo huo hispania imetangaza kwamba inawarejesha waafrika 70 nchini Morocco kama sehemu ya sera yake mpya ya kuwarejesha watu wanaingia kinyume na sheria katika eneo la Melilla au Ceuta.

Naibu waziri mkuu wa hispania Maria Teresa Fernandez De La Vega ametoa tangazo hilo alipotembelea Ceuta ambako watu watano walikufa wiki iliyopita wakijaribu kuingia katika eneo hilo.