1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

QUITO. Lucio Gutierrez bado yupo nchini Ecuador.

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKb

Kiongozi aliyeng’olewa mamlakani wa Ecuador Lucio Gutierrez amepewa hifadhi ya kisiasa na Brazil, lakini hadi kufijkia sasa utawala wa Ecuador haujamruhusu kiongozi huyo kuondoka kutoika nchini humo.

Lucio Gutierrez anaripotiwa kuwa bado yumo katika ubalozi wa Brazil nchini Ecuador mahali alikokimbilia tangu siku ya jumatano baada ya bunge la congress la nchi hiyo lilipo pitisha kura ya kumvua madaraka ya urais.

Habari zinaeleza kwamba Brazil imetuma ndege ya helicopter katika ubalozi wake mjini Quito ili kumchukua kiongozi huyo aliyeng’olewa mamlakani.

Aliyekuwa makamu wa rais wa Ecuador Alfredo Palacio sasa ndie rais mpya, na kwa mujibu wa waziri mpya wa mambo ya nje wa Ecuador Mauricio Gandara amesema kuwa Palacio atatawala kwa muda wa miaka minne iliyobaki hadi mwaka 2007 kutoka Guiterrez achukue madaraka.