PYONGYANG : Mamia wafariki kutokana na mafuriko
15 Agosti 2007Matangazo
Korea Kaskazini imeomba msaada wa kigeni baada ya mafuriko makubwa kuuwa mamia ya watu na wengine hawajulikani walipo pamoja na kusomba majengo mengi.
Shirika la habari la taifa limesema repoti za awali zimedokeza kwamba zaidi ya nyumba 30,000 zimeharibiwa kabisa au kuharibiwa vibaya.Limesema madaraja na njia za reli pia zimeharibiwa kutokana na mafuriko hayo yaliosababishwa na mvua ya karibu wiki nzima.Jimbo lililoathirika zaidi linatajwa kuwa ni la Kangwon lilioko kwenye mpaka wa kaskazini wa nchi hiyo.
Mji mkuu wa Pyongyang pia umeathiriwa na maelfu kwa maelfu ya heka za mashamba zimefurika maji.