Putin: Mazungumzo yanawezekana, lakini bila Zelensky
29 Januari 2025Matangazo
"Unaweza kujadiliana na mtu yeyote, lakini kwa sababu yeye hana sifa, hana haki ya kusaini chochote. Lakini ikiwa anataka kushiriki kwenye mazungumzo, nitawatuma watu wanaofaa ambao watafanya mazungumzo haya." amesema Putin.
Amesema kiongozi huyo wa Ukraine si halali kwa kuwa muda wake wa urais uliisha wakati kulipotangazwa sheria ya kijeshi.
Putin aidha, amedai kwamba mapigano huenda yakamalizika baada ya miezi miwili ama chini ya hapo, ikiwa mataifa ya magharibi yataacha kuisaidia Ukraine.
Kiongozi huyo wa Ukraine alijibu matamshi yao ya Putin akisema "anaogopa" mazungumzo na alikuwa akitumia "hila za kijinga" kurefusha mzozo wa karibu miaka mitatu.