1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin avunja ukimya kuhusu kifo cha Prigozhin

Sylvia Mwehozi
25 Agosti 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amevunja ukimya wake kuhusu ajali ya ndege inayoripotiwa kumuua Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin na maafisa wengine.

https://p.dw.com/p/4VYaK
Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Kazakov/AP Photo/picture alliance

Rais wa Urusi Vladimir Putin amevunja ukimya wake kuhusu ajali ya ndege inayoripotiwa kumuua Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin na maafisa wengine.

Katika maoni yake yaliyorushwa na televisheni za Urusi, Putin ametoa rambirambi zake za dhati kwa familia za wahanga wote, na kuelezea ajali hiyo kama janga.

Aidha, Rais Putin amemtaja Prigozhin kama mtu aliyekuwa na talanta, mtu mwenye hatima ngumu na aliyefanya makosa makubwa katika maisha yake lakini pia akimsifu kuwa mtu aliyetoa matokeo yanayohitajika. Ameongeza kuwa uchunguzi wa ajali hiyo utachukua muda, lakini utafanywa kwa ukamilifu na kufikia tamati.

Shirika la usafiri wa anga la Urusi lilisema kuwa Prigozhin pamoja na kamanda wa juu wa kundi la Wagner Dmitri Utkin, walikuwa miongoni mwa abiria 10 waliofariki kwenye ajali ya ndege iliyoanguka Jumatano.