1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT AU PRINCE-Wanajeshi wawili wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani wauawa nchini Haiti.

21 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUs

Wanajeshi wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti,mmoja kutoka Sri Lanka na mwengine kutoka Nepal,wameuawa wakati wa mapigano na waasi,ambao walikuwa ni wanajeshi wa zamani wa Haiti,ambao wanamiliki baadhi ya maeneo nchini humo.

Wanajeshi hao wawili wanakuwa ni askari wa awali wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kuuawa,tangu vikosi vya kimataifa kupelekwa nchini Haiti mwezi Juni mwaka jana kutuliza hali ya machafuko,baada ya aliyekuwa Rais wa Haiti Jean-Bertrand Aristide kulazimishwa kwenda uhamishoni nje ya nchi mwezi Februari mwaka jana.

Umoja wa Mataifa una kikosi chenye wanajeshi pamoja na polisi wa kulinda amani kutoka mataifa mbalimbali wanaofikia7,400 nchini Haiti.