1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHong Kong

Polisi Hong Kong yatoa zawadi kwa habari juu ya wanaharakati

14 Desemba 2023

Polisi Hong Kong imewashutumu wanaharakati watano walioko ng'ambo kwa kukiuka sheria ya usalama wa taifa iliyowekwa na serikali kuu ya China na kutoa zawadi ya dola 128,000 kwa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwao.

https://p.dw.com/p/4aADR
Hongkong | Wanaharakati wa Hong Kong
Picha za wanaharakati watano wa Hong KongPicha: Tyrone Siu/REUTERS

Waranti hizo za kukamatwa zimetolewa dhidi ya Johnny Fok na Tony Choi, wanaoendesha kituo cha mtandao wa You Tube kinachoangazia matukio ya sasa na mwanaharakati wa demokrasia Simon Cheng, Hui Wing-ting na Joey Siu.

Polisi ilikataa kutoa habari kuwahusu watano hao, lakini wasifu wao kwenye mitandao ya kijamii na taarifa za awali za vyombo vya habari, ziliashiria kuwa wamehamia Marekani na Uingereza.