Polisi Tanzania yadai muuaji wa maafisa usalama ni gaidi
2 Septemba 2021Matangazo
Mwanamme huyo aliyetambulishwa kama Hamza Mohammed, mnamo Agosti 25 aliwafyatulia risasi polisi wawili kwa kutumia bastola mjini Dar es Salaam, kisha akawapokonya bunduki zao na kuelekea kwenye ubalozi wa Ufaransa, ambako alimuuwa mlinzi.
kurugenzi wa Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Uhalifu nchini Tanzania (CID) Camilius Wambura, amesema uchunguzi wao umebainisha kuwa Hamza alikuwa gaidi.
Wambura amesema Hamza alikuwa akitazama mitandaoni ujumbe wenye misimamo mikali kutoka makundi ya kigaidi kama Al-Shabaab na lile linalojiita Dola la Kiislamu (IS).
Aidha, kulingana na maelezo ya mkuu huyo wa CID, mshambuliaji huyo alikuwa na mawasiliano na watu kutoka mataifa yenye vitendo vya kigaidi.