1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland yaadhimisha miaka 80 tangu Uasi wa Warsaw

1 Agosti 2024

Poland hii inaadhimisha miaka 80 tangu kulipozuka Uasi wa Warsaw mwishoni mwa Vita Vya Pili vya Dunia.

https://p.dw.com/p/4j0eZ
Uasi wa Warsaw
Zaidi ya raia 30 wa Kipoland waliuawa katika kipindi cha siku kadhaa mwaka wa 1944Picha: picture-alliance/dpa

Agosti Mosi, 1944, wanajeshi hao wakiongozwa na Jeshi la Kitaifa walipambana na vikosi vya NAZI kwa lengo la kuikomboa Warsaw dhidi ya uvamizi wa Wajerumani.

Soma pia: Ujerumani kuilipa fidia Poland kwa madhila yaliyosababishwa na Wanazi wa Ujerumani wakati wa vita vya pili vya dunia.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliyehudhuria hafla hiyo, ameomba radhi kwa madhila waliyopitia Wapoland mikononi mwa watawala wa kinazi wa Ujerumani. "Frank-Walter Steinmeier: Ndugu wastaafu, kila neno litakuwa ni dhaifu sana kuelezea unyama huu. Ndio maana nataka kusema sentensi moja tu. Inatoka moja kwa moja kutoka moyoni: Ninaomba msamaha. Utaifa, ubeberu na ubaguzi wa rangi ulisababisha ukatili ambao Wapoland walilazimika kujitetea kwa Uasi wa Warsaw. Hili halipaswi kutokea tena."

Ingawa uasi huo ulishindwa, lakini Rais wa Poland Andrzej Duda ameutaja kama "msingi wa maadili ya uhuru wa Poland" wakati wa hafla ya kumbukumbu hiyo jana Jumatano.